Bunge maalum la katiba leo April 25 linahairishwa bila kupitisha ibara hata moja kati ya 240 ambazo zimo katika rasimu ya katiba bunge hili linahairishwa mpaka mwezi Agosti mwaka huu huku likiendelea kujadili sura ya kwanza na ya sita yenye jumla ya ibara 19 zinazohusu masuala yanayojega msingi wa aina ya muungano unayopendekezwa.
Tume ya mabadiliko ya katiba katika rasimu ya katiba iliyowasilishwa bungeni na aliyekua Mwenyekiti wake Jaji Warioba ilipendekezwa muundo wenye shirikisho la serikali 3,pendekezo ambalo bado limeleta mtafaruku bungeni baada ya kutengeneza pande mbili bungeni kutokana na mgawanyiko huo kauli zenye utata,kejeli,matusi,dhihaka na ubaguzi ni mambo yanayojitokeza sana kwenye sura hizo mbili.
Miongoni mwa vitu vinavyolaumiwa kwa bunge hili la katiba ni matumizi ya lugha zisizofaa kwenye uchangiaji bila kujali kuwa bunge hilo linatazamwa na watu wa rika mbalimbali.