Mbunge wa Kongwa Job Ndugai leo amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ndugai alikuwa Naibu Spika wa Bunge la 10 huku Anna Makinda akiwa spika wa bunge hilo.
Akitangaza matokeo hayo Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge alisema Ndugai ameshinda baada ya kupata jumla ya kura 254 sawa na 70% kati ya kura 365 zilizopigwa.
Katika kura zilizopigwa leo na wabunge mbalimbali Ndugai alikuwa akiwania nafasi hiyo na wagombea wenzake saba huku Goodluck Ole Medeye akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 109.
Mbunge wa Kongwa Mh.Job Ndugai amepitishwa na wabunge kuwa Spika wa bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokeamatukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.