Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson leo Desemba 10, 2022 amefanya uzinduzi rasmi wa zoezi la huduma ya matibabu ya macho kwa Wananchi wa Mkoa wa Mbeya wanaofanyiwa vipimo na kupewa matibabu ikiwemo oparesheni ndogo za macho, kutoa miwani bure na uchunguzi wa awali wa mtoto wa jicho.
Huduma hiyo ambayo imeanza kutolewa rasmi jana Disemba 9, 2022 katika Shule ya Msingi Kagera iliyopo Kata ya Ilomba Jijini Mbeya ambapo huduma hizo zinatolewa bure kwa kushirikiana na taasisi ya Tulia Trust Pamoja na taasisi ya Bilal Muslim Mission Tanzania inatarajiwa kuhitimishwa siku ya kesho Disemba 11, 2022.