Burkina Faso imeweka maeneo ya Kaskazini na sehemu ya katikati ya Mashariki mwa nchi chini ya amri ya kutotoka nje ili kuzisaidia juhudi za kupambana na makundi ya wapiganaji wenye itikadi kali.
Taarifa ya Katibu Mkuu ya serikali ya jimbo la Kaskazini, Kouilga Albert Zongo imesema chini ya mpango wa kupambana na ugaidi amro ya kutotoka nje usiku itaanza kutekelezwa kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi na moja alfajiri kuanzia tarehe 3 hadi tarehe 31 mwezi Machi.
Amri hiyo pia imepiga marufuku magari na pikipiki kuwepo barabarani ndani ya muda huo uliotolewa amri hiyo itaisadia jeshi kupambana na ugaidi katika eneo hilo linalopakana na Mali kulikoanzia uasi mwaka 2015.