Damini Ogulu, anayejulikana kama Burna Boy, msanii wa Nigeria aliyeshinda Grammy, ameeleza kwa nini “anachukiwa” katika tasnia ya muziki.
Anadai kwamba “wadogo” zake wanamdharau kwa sababu hakuwa na “wakubwa”.
Mwimbaji huyo mwenye utata alichapisha haya kwenye ukurasa wake wa X siku ya Jumamosi alipoandika, “Ninachukiwa na wadogo zangu kimuziki kwa kutokuwa na wakubwa,” huku akishiriki picha yake.
Ikumbukwe kwamba Burna Boy amedai mara kwa mara kwamba anachukiwa na watu wengi haswa raia kutoka taifa lake la Nigeria.
Burna Boy alisema katika wimbo wa ‘Thank You,’ kutoka kwa albamu yake ya sasa, I Told Them, kwamba Wanigeria hawamshukuru vya kutosha licha ya kuifanya nchi hiyo kujivunia “kila nafasi ninayopata.”
Alisema badala ya Wanigeria kuthamini mchango wake mkubwa wa kimuziki kwa taifa, walieneza uvumi kuwa mama yake alikuwa mmoja wa wacheza densi wa marehemu wa Afrobeat, Fela Kuti, na kwamba ukosefu wa nguvu za kiume unaweza kuwa sababu ya yeye kutokuwa na baby mama kama wenzake wengi.
Msanii huyo wiki chache zilizopita aliwataka waaandishi wa habari za mitandaoni wote kukoma kuandika habari zake, akiashiria kwamba alikuwepo radhi kuwalipa kiasi chochote cha fedha ili kukoma kabisa kulitaja jina lake kwenye habari zao.
Kwenye akaunti yake ya X, awali ikijulikana kama Twitter mnamo Ijumaa, Burna Boy aliandika, “How far. wote hawa Instablog, PulseNg e.t.c, wanafanya mkutano wote kisha waamue ni kiasi gani nitawapa wote kuwafanya msahau jina langu kabisa.
Najua sema sijawahi kulipa hata kabla kwa hivyo nasema fanya niendeshe mwishowe. Nawasalimu ndugu zangu!!”