London iliwashwa moto wa burudani siku ya Jumapili wakati mkali wa muziki wa Nigeria, Burna Boy, akiweka historia ya kuwa msanii wa kwanza wa Kiafrika kuwa na kichwa cha habari katika uwanja wa Uingereza.
Huku mashabiki 80,000 wakihudhuria, tamasha lake umati wa watu ulionesha shauku wakisubiri onyesho hilo kwa hamu, post mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii yalionekana.
Kuanzia wimbo wake wa awali wa “Like to Party” hadi wimbo wa “Last Last”, Burna Boy ali perform orodha iliyohusisha maisha yake.
Katika kipindi chote cha onyesho la saa mbili lililofanyika katika viwanja vya klabu ya soka ya West Ham United, Burna Boy alijumuika na mastaa na nyota mbalimbali wakiwemo Stormzy, J Hus, Dave, na Popcaan.
Tamasha kuu la Burna Boy halikuonyesha tu talanta yake ya ajabu lakini pia lilitumika kama sherehe yenye mabadiliko ya kimataifa ya muziki wa Kiafrika.
Rekodi za Burna zinamfanya kuwawa kipekee ambapo amesalia kuwa msanii pekee kutoka Afrika anayezungumziwa duniani