Wizara ya Biashara ya Burundi imepiga marufuku uagizaji mahindi kutoka nje kwa miezi sita kuanzia Machi 8, Mwaka huu.
Katika taarifa wizara hiyo imesema mahindi yaliyoingizwa nchini humo hivi karibuni ”hayakua mazuri” na huenda yakadhuru afya ya watu.
Aidh, taarifa hiyo haikubainisha mahindi hayo yaliagizwa kutoka nchi gani.
”Wakati nafaka hii na unga inakataliwa na nchi jirani… tunahitaji kuhakikisha hayaingizwi nchini”, alisema Jeremie Banigwaninzigo, katibu wa kudumu wa wizara ya biashara na utalii wa Burundi.