Serikali ya Burundi imetangaza kuwa katika wakati mgumu na kutangaza hali ya hatari kutokana na kujaa kwa Ziwa Tanganyika na kuingia katika makazi ya watu.
Waziri wa Mambo ya Ndani Martin Niteretse amfahamisha kuwa hadi kufikia sasa zaidi ya watu 200,000 wameyakimbia makazi yao huku zaidi ya elfu ishirini wakiwa hawana sehemu ya kulala kabisa.
Burundi imeyataka Mataifa kuisaidia kutokana na maafa hayo ambayo yameonekana kuwa makubwa kwa nchi.
Katika kata ya Gatumba tangu kunyesha kwa mvua za El Nino watu saba wamefariki Dunia wengine wakiwa hawajulikani walipo baada ya kusombwa na maji wengi wao wakiwa ni watoto.