Busta Rhymes anatazamiwa kutambuliwa kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu na kupokea Tuzo za uvumbuzi na uongozi za mwaka 2023.
Hili ni tukio la saba la kila mwaka litaadhimisha kama kumbukumbu ya miaka 50 ya Hip Hop mwaka huu litakalofanyika Juni 24 huko Beverly Hilton huko Los Angeles na kuangazia mchango wa kipekee wa Busta kwenye tasnia hiyo.
“Kama gwiji wa kufuatilia na mwenye maono ndani ya muziki wa Hip Hop, Busta Rhymes ametoa mchango usio na kifani unaofanya yeye kuwa na vigezo na sifa anyostahili tuzo,” shirika liliandika katika taarifa kwa vyombo vya habari.
Joi Brown, mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Culture Creators, aliongeza: “ Tuzo za Innovators and Leaders Awards Brunch mwaka huu ina umuhimu usio na kifani tunapoadhimisha kumbukumbu ya miaka 50 ya Hip Hop. Tunayofuraha kuwapa heshima watu wa kipekee ambao wameleta chachu za tamaduni za Weusi na Hip Hop huku pia tukionyesha uwezo wa kudumu wa jambo hili la kitamaduni la kimataifa’.
Wapokeaji wa Tuzo hizo ni pamoja na marehemu Andre Harrell, Russell Simmons, Sylvia Rhone, Byron Allen, Swizz Beatz na L.A. Reid.
Chloe x Halle pia atatunukiwa mwaka huu, akipokea Tuzo ya Wavumbuzi wa Mwaka.[Innovators of the Year Award].
Umekuwa mwaka mzuri kwa gwiji wa Busta Rhymes. Mwezi uliopita, yeye na Janet Jackson hatimaye walipata fursa ya kutumbuiza wimbo wao wa pamoja wa 1998 “What’s It Gonna Be?!” kwa mara ya kwanza. Muda huo yalifanyika huko Madison Square Garden wakati wa ziara ya Jackson Together Again Tour.
Mnamo Machi, Busta katika onyesho maalum lililoungwa mkono na orchestra katika Ukumbi wa Carnegiena wakati fulaani, alichukua muda wake kuongea na mashabiki zake na kuwaambia watazamaji jinsi ilivyokuwa nafasi nzuri na ya kipekee kwake kuwa mtoto kutoka Brooklyn akiigiza huko Carnegie Hall na mama yake akimsaidia wakat huo.
“While she was making breakfast, I used to see Transformers and Voltron,” he shared with the sold-out audience, noting that his cartoons would come on between 6:30 and 8:00 am.