Rais wa Liberia George Weah ameagiza kutolewa kwa kipengele kinachoonyesha ubaguzi kwenye katiba ya nchi hiyo, ambacho kinaruhusu upatikanaji wa uraia kwa watu weusi tu.
Ametoa agizo hilo katika hotuba yake ya kwanza kwa Waliberia tangu achaguliwe kuwa Rais. Weah amesema vikwazo na vipingamizi vyote hivi viliwekwa wakati ambao havikuwa vinahitajika tena.
Namnukuu Weah “Kipengele hicho ni cha kibaguzi na hakina maana yoyote”
Katiba ya Liberia inamtambua mtu mweusi kwa jina la ”Negro” jina la kibaguzi walilokuwa wakiitwa watu weusi wakati wa utumwa.
George Weah ameahidi pia kufuta sheria inayowazuia wenyeji kumiliki ardhi. Watu kutoka mataifa mbalimbali hasa raia 4,000 wa Lebanon wanaishi nchini Liberia kwa miaka kadhaa, lakini wamenyimwa uraia na haki ya kumiliki ardhi.
LIVE: UZINDUZI WA HATI UA KUSAFIRIA YA KIELEKTRONIKI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA