Mahakama ya Katiba nchini Gabon imemuamuru Waziri Mkuu wa nchi hiyo kujiuzulu na kuvunja bunge baada ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika weekend iliyopita kuchelewa.
Mahakama hiyo imeeleza kuwa Waziri Mkuu huyo Emmanuel Issoze-Ngondet na bunge la nchi hiyo halitambuliki tena kwasababu walichelewa kufanya uchaguzi kwa mujibu wa sheria.
Pia mahakama hiyo imemuamuru Rais wa nchi hiyo Ali Bongo kumtangaza Waziri Mkuu wa Mpito mpaka hapo uchaguzi utakapopangwa.
BIRTHDAY YA SUGU: Surprise aliyofanyiwa na Mkewe gerezani