Leo July 8, 2018 Kuna hii ya kuifahamu ni Umoja wa wazee nchini Kenya umeitaka Serikali kuondoa kwenye vitambulisho vya taifa sehemu zinazoonesha mahali ambapo mhusika amezaliwa kwani inaleta ukabila.
Kenya ni taifa linalokabiliwa na hali ya ukabila hususani kwenye siasa na kazi, hali inayosababisha anayechaguliwa kuongoza au kupewa kazi wakati mwingine kuathiriwa na mahali alipozaliwa.
Muasisi wa umoja huo, Martin Kinyanjui amesema kuwa wazee wameamua kuungana kuhakikisha wanajenga umoja wa kitaifa bila kutumia siasa.
“Umoja huu ulitakiwa kuanzishwa mwaka 2016 lakini kwa sababu hatukutaka kamwe kujihusisha na masuala ya siasa, tulilazimika kusubiri hadi michakato ya uchaguzi ikamilike,” alisema Kinyanjui.
MAGAZETI LIVE: Mwigulu amwaga mboga, Kauli 3 tata za Lugola