Rais John Magufuli katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Kidatu Ifakara mkoani Morogoro leo May 4, 2018 ametahadharisha wakandarasi na watendaji wanaokula hela za serikali za miradi ya maji mkoani humo.
Ameagiza wakandarasi hao ambao wamekula fedha hizo za miradi ya maji Morogoro waanze kushughulika ili maji yapatikane haraka iwezekanavyo, au warudishe fedha hizo, la sivyo watahukumiwa kisheria.
Rais Magufuli ameeleza kuwa wakandarasi hao wanaweza kuhukumiwa hadi miaka mitano jela kwa sheria namba 17 ya mwaka 1997 ya Makandarasi kwa kula fedha za miradi hiyo.
“Makandarasi waliokula fedha za mradi, wamekula sumu, hela za serikali haziliwi, ni nafuu ukale sumu ila sio pesa za serikali ya awamu ya tano.” – Rais Magufuli
Agizo alilolitoa Waziri Ndalichako Bungeni “huo ni uhalifu”