Taarifa zilizotufikia hapa Ayo TV na millardayo.com ni kwamba mkoani Kilimanjaro katika wilaya ya Mwanga ni mtoto Hashim Ally Msuya ambaye ni wa umri wa miezi tisa amechinjwa na mama yake mzazi.
Mama huyu aliyetambulika kwa jina la Hadija Msangi alimchinja mwanaye huyo akiwa chumbani na kisha kumuweka ndani ya mfuko wa salfeti na kisha khifadhi chini ya kitanda. Mpaka sasa mwili wa mtoto umekwisha fanyiwa uchunguzi na umeshakabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issah ameeleza kuwa mwanamke huyu tayari anashikiliwa na Jeshi la Polisi na kuwa inadaiwa mama huyu ana tatizo la ugonjwa wa akili.
Kamanda Issah pia amegusia matukio mengine ikiwa ni pamoja na la mwanamke aliyepotea na kukutwa amedumbukia kwenye korongo na lile la kifo cha Mwenyekiti wa Kitongoji cha Miembeni Wilaya ya Hai baada ya kukutwa kwenye kibanda cha kuuza samaki akiwa amefariki bila kuwa na jeraha lolote.
Alichokibaini Naibu Waziri Mavunde katika ziara ya kushtukiza Mwanza
“Hukumu ya Sugu tuliijua siku nyingi na imepangwa Hotelini” -Mbowe