Tume ya Ushindani nchini FCC imesema katika kipindi cha miaka mitatu imepokea zaidi ya malalamiko 600 ya Walaji na watumiaji wa bidhaa mbalimbali ambapo malamiko 550 yanahusu uwepo wa bidhaa bandia katika soko nchini ambazo zimesababisha hasara kubwa kwa taifa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma kuhusu maadhimisho ya siku ya ushindani duniani yanayotaraji kufanyika December 5 mwaka huu Mkurugenzi Mkuu wa tume ya ushindani nchini FCC Dr. John Mduma amesema tume hiyo imeandaa mikakati mbalimbali ya kuhakikisha inapambana na soko la ushindani kwa kudhibiti uingizwaji wa bidhaa feki kupitia kwenye Bandari na maeneo ya mipakani.
DC SABABYA AMSWEKA NDANI MENEJA ANAELIPWA MILIONI MOJA NA NUSU, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA.