Mbunge wa Kilwa Kusini Selemani Bungara (Bwege) ametangaza kuondoka CUF na kuhamia rasmi ACT Wazalendo ”ninawatangazia rasmi kuwa likivunjwa Bunge tu mimi sio tena Mwanachama wa CUF ,karibuni ACT”
“Nahamia ACT kwasababu Chama kina miaka mitano na hakijafikia hatua ya kwenda kinyume na Katiba ukiingia sasa hivi ni ile kambare mkunje angali mbichi, ukibaki CUF, CCM makovu ndio hayohayo, kwahiyo najiunga ACT kukipika kabla hakijaharibikiwa”-BWEGE
“Mimi sio Mfuasi wa Maalim Seif, ni Mwanasiasa mkongwe najua maana ya siasa, sijamfuata Maalim Seif, nilikuwa CUF ya Maalim Seif nikiisimamia Katiba ya CUF, kitendo cha Lipumba kujiuzulu na kulazimisha kurudi CUF niliona hafai kuwa Kiongozi” – BWEGE