Tukiwa tunaelekea katika uchaguzi mkuu wa club ya Simba SC, Jumapili ya October 28 2018 mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa club hiyo, Swed Mkwabi amezindua rasmi kampeni na kunadi sera zake.
Swed Mkwabi amezindua rasmi kampeni na kuanza kunadi sera zake kuhusiana na vitu atakavyofanya kama wana Simba SC wakiamua kumpa ridhaa ya kuiongoza club hiyo katika uchaguzi mkuu.
“Nikipita tutaangalia sehemu zenye mianya kwa kushirikiana na TFF na bodi ya Ligi ili kumaliza ujanja ujanja magetini, kwanza nitakachokifanya nitajaribu kuongea na TFF ule mfumo wa kielectronic umekwamia wapi”-Mkwabi
“Naamini kila siku zinavyokwenda kuna uboreshaji kwa maana tukiangalia nje kuna siti namba na kila mtu ana tiketi yake, sasa tukitumia utaratibu huo naamini tunaweza tukatatua hilo tatizo”-Mkwabi