Shirikisho la soka Afrika CAF limetangaza kuahirishwa kwa fainali za michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).
CAF imetangaza kuahirisha fainali hizo ikiwa zimesalia siku chache kabla ya kuanza April 4 na kumalizika April 25 nchini Cameroon, wameahirisha hivyo kutokana na kuenea kwa virusi vya corona.
Hata hivyo kabla ya taarifa hizo kutoka ambapo Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi shiriki, timu ya taifa ya Morocco na Rwanda zilitangaza kujitoa kwa hofu ya virusi vya corona.