Shirikisho la soka Afrika (CAF) limekataa ombi la Biashara United lililotumwa CAF kupitia TFF la kutaka mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya kusogezwa mbele.
Ombi hilo lilitumwa CAF baada ya Biashara United kushindwa kusafiri kwa ndege ya kukodi kutoka Tanzania kwenda Libya sababu ya kukosa vibali vya kimataifa vya kutumia anga ya Sudan, Sudan Kusini na kutua Benghazi.
Hivyo kutokana na ombi hilo kukatataliwa licha ya ushindi wa 2-0 walioupata Dar es Salaam, Al Ahly Tripoli inaaripotiwa kuwa na uwezekano mkubwa wa CAF kutangaza kuwa inasonga hatua inayofuata kwani biashara anahesabika hajatokea uwanjani.