Muamuzi Mohamed Ali Adelaid amefungiwa miezi mitatu kuchezesha soka na shirikisho la soka Afrika (CAF) baada ya kuchezesha kiwango cha chini.
Adelaid raia wa Comoro amepewa adhabu hiyo baada ya kuchezesha chini ya kiwango mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2021 kati ya Algeria na Zambia March 25 2021 kiasi cha FA ya Algeria kupeleka malalamiko CAF.
Kwenye mchezo huo ambao Zambia alikuwa mwenyeji ulimalizika kwa kufungana magoli 3-3, ambapo katika Kundi lao H amefuzu Algeria na Zimbabwe.