Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF huwa linautamaduni wa kutoa Tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kila mwaka, kama ambavyo Shirirkisho la mpira wa miguu barani Ulaya UEFA wanavyokuwa wanaandaa Tuzo ya mchezaji bora Ulaya, basi Afrika huwa wanaandaa Tuzo hizo kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika na nje ya Afrika.
November 2 wametangaza Top 10 ya majina yaliofanikiwa kuingia katika Top 10 hiyo kwa wachezaji wa ndani na nje ya Afrika. Good news ni kuwa mtanzania Mbwana Samatta ambaye anakipiga katika klabu ya TP Mazembe ndio mchezaji pekee kutoka Afrika Mashariki aliyekuwemo katika list hiyo, Hii ni List ya majina 20 ya wachezaji waliochaguliwa kuingia katika Top 10 ya wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika na Top 10 ya wachezaji wanaocheza nje ya Afrika.
- Abdeladim Khadrouf (Morocco & Moghreb Tetouan)
- Baghdad Bounedjah ( Algeria & Etoile du Sahel)
- Felipe Ovono (Equatorial Guinea & Orlando Pirates)
- Kermit Erasmus (South Africa & Orlando Pirates)
- Mbwana Aly Samatta (Tanzania & TP Mazembe)
- Mohamed Meftah ( Algeria & USM Alger)
- Mudather Eltaib Ibrahim ‘Karika’ (Sudan & El Hilal)
- Robert Kidiaba Muteba ( DR Congo & TP Mazembe)
- Roger Assalé (Cote d’Ivoire & TP Mazembe)
- Zineddine Ferhat (Algeria & USM Alger)
Top 10 ya wachezaji wanaocheza nje ya Afrika
- André Ayew (Ghana & Swansea)
- Aymen Abdennour (Tunisia & Valencia)
- Mudather Eltaib Ibrahim ‘Karika’ (Sudan & El Hilal)
- Mohamed Salah (Egypt & Roma)
- Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund)
- Sadio Mané (Senegal & Southampton)
- Serge Aurier (Cote d’Ivoire & Paris Saint Germain)
- Sofiane Feghouli (Algeria & Valencia)
- Yacine Brahimi ( Algeria & Porto)
- Yaya Touré (Cote d’Ivoire & Manchester City)
Namna ya kumpata mshindi wa tuzo hiyo ni kwa njia ya kupiga kura kwa makocha wa timu za taifa au wakurugenzi wa ufundi wa mashirikisho wanachama wa CAF. Tuzo hizo za mchezaji bora wa Afrika kwa 2015 zitatolewa Alhamisi ya January 7 2016 Abuja Nigeria.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.