June 24 2016 shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza maamuzi magumu ya kuitoa klabu ya ES Setif ya Algeria katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, katika hatua ya nane bora hivyo kufanya Kundi B libaki na timu za Enyimba, Mamelodi Sundowns na Zamalek.
CAF wamefikia maamuzi hayo baada ya kukaa chini na kupitia vifungu vya sheria, ni adhabu gani inastahili kwa klabu hiyo, ambayo imetolewa katika mashindano hayo kwa kosa la mashabiki wake kufanya fujo katika uwanja wao wakati wa mchezo dhidi ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini June 19 2016.
Kufuatia vurugu zilizotokea katika mechi no. 98 ya Klabu Bingwa Afrika 2016 kati ya ES Setif ya Algeria dhidi ya Mamelodi Sundowns ya South Africa, mwamuzi aliamua kumaliza mchezo kabla ya muda, kwa mujibu wa kanuni kama mwamuzi akimaliza mchezo kwa sababu ya vurugu za za mashabiki wa timu mwenyeji, basi watakuwa wamepoteza mchezo.
GOAL AND HIGHLIGHTS: MO BEJAIA VS YANGA JUNE 20 2016, FULL TIME 1-0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE