Yanga ndio klabu pekee inayoiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika hatua ya Makundi, headlines zimekuwa nyingi toka Yanga wanaojiandaa na mchezo wao wa pili wa hatua hiyo, kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya MO Bejaia ya Algeria na kupoteza kwa goli 1-0.
Headlines zimekuwa nyingi baada ya Yanga kucheza mchezo wao wa kwanza wakiwa na jezi tofauti na tulizozizoea, kutokana na zile za kwao kukataliwa na CAF huku Yanga wakiwalaumu TFF, June 24 2016 afisa habari wa TFF Alfred Lucas ameweka wazi ukweli.
“Yanga walivyoingia hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho TFF waliendelea kuisaidia Yanga kwa kila kitu ili ishiriki vizuri, lakini CAF walitoa barua a kuwaambia Yanga waende watu watatu Cairo kwenye semina ili kufahamishwa taratibu na upatikanaji wa vifaa lakini Yanga hawakwenda”
GOAL AND HIGHLIGHTS: MO BEJAIA VS YANGA JUNE 20 2016, FULL TIME 1-0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE