Takwimu zinaonesha kuwa kila mwaka watu milioni 1.6 duniani hufariki kwa saratani ya mapafu moja ya sababu kubwa ikiwa ni uvutaji wa sigara.
Hatahivyo wanasayansi wamegundua kifaa cha kimtandao (Calculator), ambacho kinaweza kupiga hesabu kama mtu yuko kwenye hatari au ana dalili za kupata saratani ya mapafu katika kipindi cha miaka 6 hadi 16 ijayo.
Kifaa hicho kimepewa jina la ‘great idea‘ na kimethibitisha ubora wake kwa kutoa usahihi kwa asilimia 90 katika majaribio yote ya saratani yaliyofanyika.
Deborah Arnott ambaye ni Mtendaji Mkuu wa mfuko wa Health Charity Action on Smoking and Health aliiambia MailOnline kwamba ni wazo zuri sana kuleta kifaa hicho ‘Calculator‘ cha kupima saratani ya mapafu.