Umoja wa Mataifa umesema kuwa ongezeko linalokuja la chanjo ya malaria barani Afrika litakuwa mkombozi katika vita dhidi ya ugonjwa huo, baada ya shehena ya kwanza ya dozi kuwasili nchini Cameroon.
Kwenye taarifa ya pamoja, Shirika la afya duniani WHO, UNICEF na kampuni ya chanjo ya Gavi, yamesema dozi hizi zaidi ya laki tatu, zinaashiria kuwa utoaji chanjo dhidi ya Malaria utaongezeka katika maeneo hatarishi zaidi barani humo.
Chanjo aina ya RTS,S ndiyo chanjo ya kwanza ya Malaria iliyopendekezwa na WHO, na inatolewa katika dozi nne, ya kwanza ikitolewa kwa watoto walio na umri wa miaka mitano, kukabiliana na kimelea cha plasmodium Falciparum ambacho ni hatari na kilichoenea zaidi barani Afrika.
Ndani ya wiki kadhaa zijazo, dozi zingine milioni 1 na laki 7 zitatolewa kwa nchi za Burkina Faso, Liberia, Niger na Sierra Leone.