Baada ya kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa January 10 kuamua kutangaza kumvua unahodha Nadir Haroub Canavaro na kutangaza kumpatia nafasi hiyo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta, hali imekuwa tofauti kwa upande wa Canavaro.
Canavaro ambaye ameichezea timu ya taifa ya Tanzania kwa takribani miaka 10, ameamua kutangaza kustaafu kucheza timu ya taifa, Canavaro ametaja sababu kadhaa zilizomfanya afikie maamuzi hayo, ikiwemo sababu ya kuvuliwa unahodha bila ya heshima yoyote, licha ya kuitumikia timu hiyo kwa muda mrefu.
“Sing’ang’anii na wala silazimishi kuwa nahodha, kikubwa ninachotaka ni kupewa heshima yangu kwa kuipeperusha vyema bendera ya timu ya taifa, Kiukweli nimepokonywa unahodha bila ya heshima, ninajisikia vibaya kupokonywa unahodha kwa kupitia vyombo vya habari kitu ambacho siyo sahihi, hali hiyo imeshusha heshima yangu kwa kiwango kikubwa” >>> Canavaro
Hata hivyo Canavaro ametaja sababu nyingine iliyomfanya kuamua maamuzi ya kujitoa Taifa Stars, kwani baada ya mechi ya ugenini iliyochezwa dhidi ya Algeria na Taifa Stars kufungwa goli 7-0, lawama na maneno maneno yalimuangukia yeye kuwa ameisha na umri umemtupa mkono hivyo ameona awaachie vijana waendele kuichezea Taifa Stars.
CHANZO CHA HII STORI: Salehjembe
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.