Leo June 2018 Nakusogezea hii kutoka nchini Canada ambapo kwetu Bangi ikiwa ni haramu wenzetu wamepitisha sheria rasmi kwa nchi nzima inayoruhusu matumizi ya bangi kwa raia wa nchi hiyo na hata wageni.
Sheria imepitishwa kwa kupata kura za ndiyo 52 zinazoruhusu matumizi ya bangi hadharani, huku kura 29 za maseneta zikisema hapanana kwa kupita huko itakuwa inasimamia udhibiti, usambazaji na uuzaji wake.
Kwa sheria hiyo sasa raia wa Canada wataruhusiwa kununua na kutumia bangi kihalali kuanzia mapema mwezi September mwaka huu.
Kumiliki bangi ilikuwa ni kosa kisheria tangu mwaka 1923 lakini matumizi ya bangi kama dawa yaliruhusiwa kisheria tangu mwaka 2001.