Shirika la Care International Tanzania limeadhimisha siku ya mkulima kwa kuwatembelea wakulima na kutoa elimu ya kilimo cha soya na alizeti na katika mashamba darasa yaliyopo katika baadhi ya vijiji ikiwemo vijiji vya Tagamenda na Uhominyi iliyopo katika halmashauri ya Iringa ili kuwaondoa wakulima kulima kimazoea na badala yake kulima kilimo chenye tija .
Katika maadhimisho hayo Mratibu wa Mradi wa Farmers Field and Business School (FFBS) Ramadhani Lissu ameiambia AYOTV kuwa mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri ya Iringa katika Vijiji zaidi ya 61 ukiwa na lengo la kuwafikia wakulima takriban zaidi ya 7,700 na hadi sasa umefikia miezi 16 na umewafikia zaidi ya wakulima 7,345 na ukiwa na mashamba darasa 308 ambapo ndio lengo la mradi huo kutekeleza vipengele 6 ikiwemo kipengele cha lishe na kupinga ukatili .
Ramadhani ameendelea kusema pia vipengele vingine vinavyotekelezwa na mradi huo ni pamoja na na kutekeleza kilimo kinachoweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi , kudumiaha usawa na kuwafundisha pia wakulima namna ya kutafuta masoko na kuwaunganisha pia na wadau wa masoko.
Ramadhani amesema pia mradi huo utawafundisha pia wakulima namna ya kutengeneza bustani za nyumbani ili kuondokana kutumia mboga moja kila siku.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Stephen Mhapa amewapongeza shirika hilo la Care International kwa kutoa elimu ya mashamba darasa kwa wakulima ili kulima kilimo chenye tija na huku akiwaasa wakulima elimu waliyo patiwa wakaitumie ipasavyo.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima wanufaika na mradi huo wamekshukuru pia shirika hilo wa kuwafundisha namna bora ya ufanyaji aa shughuli za kilimo za kibiashara zaidi .