Staa wa zamani wa soka wa Liverpool Jamie Carragher ameweka wazi msimamo wake na kueleza kuwa anamuunga mkono mtendaji mkuu wa Man United Ed Woodward kwa kuahirisha kumsajili Erling Haaland katika dirisha dogo la January na Haaland kwenda kujiunga na Borussia Dortmund ambayo anaisaidia na kuifungia magoli mengi.
Haaland dili lake na Man United baada ya kufa na kujiunga na Borussia Dortmund ya Ujerumani, Dortmund ameichezea jumla ya game 7 hadi sasa kufunga magoli 11, Ed Woordward aliua mpango wa kumsajili mchezaji huyo kwakuwa wakala wake Mino Raiola alikuwa anataka pesa nyingi, hivyo Carragher haoni tatizo kufutwa kwa mpango huo.
“Kwa yeyote ambaye amemsajili Haaland kutokea RB Salzburg anatakiwa ajue sio tu amepata kipaji chipukizi lakini pia wamealika matatizo mjini kwa mfumo wa wawakilishi wake, kila club ambayo itakuwa inamtaka kinda huyo wa kinorway lazima watatakiwa kupima thamani ya mchezaji na gharama zinazoongezwa kutoka kwa mshauri wake mkuu (Raiola)”>>> Jamie Carragher
“Haijalishi Ole Gunnar Solskjaer atamshawishi Haaland kwa kiwango gani mchezaji huyo ajiunge Old Trafford lakini haina maana ushauri wa Raiola angeuzingatia zaidi mchezaji kuliko wa yoyote, siwezi kusaidia lakini nafikiri Haaland kama angekuwa anasimamiwa na mtu mwingine sasa hivi angekuwa Old Trafford”>>> Jamie Carragher
VIDEO: MECKY AGOMA KUMTUPIA ZIGO LA LAWAMA TINOCO KIPIGO CHA 1-0 CHA SIMBA