Mradi mkubwa wa maji wa thamani ya Tsh Bilioni 80 katika wilaya ya Kinondoni na maeneo mengine jijini Dar es Salaam unaendelea kutekelezwa na inaelezwa kuwa hatua iliyofikiwa sasa hadi kukamilika kwa mradi huo ni asilimia 80.
Haya yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi ambaye ameeleza kuwa wastani wa utoaji wa maji katika maeneo ya wilaya hii utaongezeka kutoka asilimia 75 hadi 95 katika maeneo ya Makongo, Changanyikeni, Mabwepande na maeneo ya Wazi Hill.
DC Hapi pia amezungumzia kero ya wananchi kupelekewa bili za maji wakati maji hayajatoka katika makazi yao na kuelekeza wananchi kuwa bili hizo zisilipwe na akawaagiza DAWASCO kulifuatilia suala hilo na kuhakikisha bili za namna hiyo zinafutwa zote ili wananchi wasiendelee kuishi kwa hofu.
“Meneja anayehusika wa DAWASCO nampa wiki mbili awe amemaliza jambo hili.” – DC Ally Hapi
Ni marufuku shule kukaririsha, kuhamisha au kufukuza wanafunzi wanaofeli” – Wizara ya Elimu
Naibu Waziri katoa onyo hili kuhusu wanafunzi watakao pewa mimba