Baada ya uchaguzi wa Umoja wa Vijana UVCCM kumalizika Dodoma, aliekuwa Mgombea wa nafasi ya uwenyekiti Thobias Mwesiga Richard amekutana na Waandishi wa Habari Dodoma na kuzungumza baada ya kushindwa kwenye uchaguzi huo.
Namnukuu akisema “Kwanza naomba kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa Chama changu kwa kunipa fursa ya kuwa kati ya Vijana 113 waliochukua fomu lakini pia kupata uteuzi kati ya vijana 7 waliopitishwa na Halmashauri kuu kugombea nafasi hiyo“
“Pamoja na hayo leo hii nimempigia simu Mwenyekiti alieshinda kumpongeza kwa kupata ushindi lakini pia kumuahidi kwamba nitampa ushirikiano wangu kwenye majukumu yake mbalimbali, pamoja na pongezi hizo yapo matendo ambayo hayakuridhia katika uchaguzi wetu“
“Mh. Rais wakati akifungua mkutano mkuu wa Umoja wa vijana alizungumza na kukemea sana vitendo vya rushwa lakini jambo hili limejitokeza, nadhani baadhi ya waliokua Viongozi wamekamatwa… jambo hili linashusha heshima ya Chama lakini nimeshukuru sana Mwenyekiti Rais Magufuli kwa kukemea kwa dhati“
“Tunaamini hatua kali za dhati hasa za kisheria zitachukuliwa hasa za kisheria kwa wale wote wataobainika walishiriki katika vitendo hivyo” – Thobias
Mtazame zaidi Mwesiga akiongea kuhusu mali za Jumuiya na anachopendekeza Mwenyekiti mpya akifanye, bonyeza play hapa chini
VIDEO: MWENYEKITI MPYA WA UVCCM APATIKANA, TAZAMA ALICHOSEMA BAADA YA KUTANGAZWA MSHINDI