CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa kimesema hakitakuwa na huruma na wawakilishi wake wa wananchi ambao hawatakuwa wakishiriki vikao mbalimbali vya chama hicho kwa madai ya kuwa na udhuru huku kikisema wanajiweka katika mazingira magumu ya kupendekezwa na chama hicho katika chaguzi zinazokuja.
Kimetoa msimamo huo leo katika kikao chake maalumu ambacho mgeni wake rasmi alikuwa Katibu wa NEC Organizesheni, Issa Haji Ussi (Gavu) kilichofanyika katika ukumbi wa Ihemi nje ya Iringa na kushirikisha wajumbe zaidi ya 700 wa halmashauri kuu za wilaya zote za kichama za mkoa huo.
Wawakilishi ambao hawakuwepo katika kikao hicho wakati tamko hilo likitolewa ni pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini Jesca Msambatavangu, wa Mafinga Mji Cosato Chumi, Kilolo-Justin Nyamoga, Isimani-William Lukuvi, na Mufundi Kaskazini-Exaud Kigahe.