CCM YAKEMEA MAKUNDI UWT, MTEMVU ATOA KAULI “MUWE WAMOJA, TUTASHINDA MITAA YOTE”
Chama Cha Mapinduzi kimewataka Umoja wanawake (UWT) kuacha makundi ya uchaguzi badala yake wajipange kuwa wamoja kabla hata awajaanza kuelekea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 na ule Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Hayo ameyazungumza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam Abbas Mtemvu wakati wa ufunguzi wa semina ya UWT ambayo imeandaliwa na Umoja wanawake UWT Wilaya ya Ilala kwa viongozi wa Kata na Matawi kwa ajili ya kuwapatia elimu ya Fedha na mikopo ,Elimu ya uwandishi wa barua ,majukumu ya uongozi na maandalizi ya Uchaguzi .
“Niwaambie tu Mwaka 2024 chama cha Mapinduzi tutashinda Mitaa yote nawataka umoja wanawake UWT kuacha vikundi na fitina nashangazwa kuona watu wapo katika Makundi wakati Uchaguzi umeisha naomba Wanawake muwe wamoja kujenga chama na Jumuiya “Amesema Mtemvu.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wanawake UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa, amewataka UWT Ilala kuwa mkombozi wa Mwanamke wafanye Siasa na uchumi katika kujenga chama na Serikali kwa pamoja kwa lengo la kujiimarisha katika nyanja zote.
Hata hivyo Mwenyekiti Neema aliwataka wanawake wa UWT washirikiane kwa pamoja kuzungumzia upendo na kukijenga chama na Jumuiya zake kabla ya kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na hata Uchaguzi Mkuu wa Rais mwaka 2025.