Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM imekutana leo December 13 2016 jijini Dar es salaam kwa kikao cha siku moja cha kawaida. Kikao hicho kimeongozwa na mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Dkt. John Magufuli. Pamoja na mambo mengine, halmashauri kuu ya Taifa imepokea taarifa ya tathmini ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Baada ya kikao hicho, aliyekuwa katibu wa NEC, itikadi na uenezi, Nape Nnauye alikutana na waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa taarifa ya maamuzi ya kikao hicho, kikubwa alichokizungumza ni pamoja na kuwa CCM ina mpango wa kuhakiki wanachama wake.
Nape amesema Halmashauri kuu imeona ipo haja ya kufanya uhakiki wa wanachama wa CCM na Jumuiya zake ili kujua idadi sahihi ya wanachama kwa wakati huu. Uhakiki huo utaendana na kutoa kadi mpya za uanachama za kielektroniki ili kuwa na udhibiti wa usahihi wa wanachama na kuondoa wanachama hewa aidha kadi za UWT, WAZAZI na UVCCM zifutwe ili ibaki kadi moja ya CCM tu.
VIDEO: Vipaumbele 10 vya Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli ndani ya CCM, Bonyeza play hapa chini kutazama