Kutokana na ukubwa wa Tukio la Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania siku ya Jumapili October 25 2015, stori zinazohusu Siasa zinakuja kila siku kwenye Headlines na kila kubwa ambayo inanifikia nahakikisha tu na wewe inakufikia wakati huohuo.
Imenifikia Taarifa kutoka Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba Dar es Salaam ambapo January Makamba, Mjumbe wa Kamati ya Kampeni CCM ameitoa Taarifa hii.
Kwenye kile alichokisema kuna hili jibu kuhusu Mgombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 anayewakilisha CCM, Dk. Magufuli kushiriki Midahalo >>> ‘CCM ilipokea mwaliko wa MCT na kuijibu tarehe 13 Septemba 2015.. CCM ilitoa kauli rasmi, iliyosainiwa, ikithibitisha kushiriki mdahalo, tunaamini ni vyema mdahalo huu ukaandaliwa na ushirika wa Taasisi mbalimbali zenye nia ya kuandaa… Magufuli amekubali kushiriki Mdahalo wa Wagombea Urais‘ >>>- January Makamba.
Jana kulikuwa na stori ambayo iligusa sana kwenye Siasa TANZANIA, ishu ni Matokeo ya Utafiti uliofanywa na Taasisi ya TWAWEZA >>> ‘CCM haikushangazwa na matokeo ya Utafiti wa TWAWEZA ambayo yanatoa ushindi wa 65% kwa Ndugu John Magufuli dhidi ya 25% za Mgombea wa UKAWA… Matokeo ya Utafiti huu ni ishara kwamba Watanzania wamemkubali na kumuelewa Ndugu Magufuli‘ >>> January Makamba.
Maneno mengine ya January Makamba haya hapa >>> ‘Mwezi Agosti 2010 Taasisi ya SYNOVATE ilitoa Utafiti ikionesha CCM itashinda Uchaguzi wa 2010 kwa 61%, Wapinzani waliwalaani na kuwashitaki SYNOVATE… Kwenye Matokeo halisi CCM ilipata Kura zilezile 61%‘ >>>- January Makamba.
Taarifa yote ninayo hapa pia kama unahitaji kuisoma mwanzo mpaka mwisho.
Picha nyingine toka ndani ya Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya CCM hizi hapa.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE