Dk. Magufuli na Mama Samia wamepewa vyeti vya Urais.. picha kuanzia ukumbini mpaka Ofisi za CCM.
Share
4 Min Read
SHARE
Jina la aliyekuwa Waziri Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli lilianza kubeba headlines za uzito zaidi kipindi ambacho na yeye alitangaza kuingia kwenye mchakato wa kugombea Urais kwa kuchukua Fomu kutoka Makao Makuu ya Chama Dodoma, baadae akateuliwa… akapita kwenye Kampeni na hatimaye matokeo ya Uchaguzi wa October 25 2015 yakampitisha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwenye picha ya pamoja, hapo ni Dk. Magufuli, Mama Samia Suluhu, Jaji Damian Lubuva na baadhi ya Wagombea waliokuwa wakigombea kiti cha Urais Tanzania kwenye Uchaguzi wa mwaka 2015.
Tume ya Uchaguzi NEC imekamilisha kazi yake ambapo leo October 30 2015 Dk. Magufulina mgombea mwenza wake ambaye atakuwa Makamu wa Rais Serikali ya awamu ya tano, Mama Samia Suluhu Hassan wamekabidhiwa rasmi vyeti vya kuthibitisha ushindi wao kwenye nafasi hizo.
Kazi ya vyeti ilikuwa pale Ukumbi wa Diamond Jubilee, eneo la Upanga Dar es Salaam na baada ya hapo msafara ukaelekea katika Ofisi za CCM zilizopo mtaa wa Lumumba , Dar es Salaam.
Naibu Spika aliyemaliza muda wake, Job Ndugai.Kamanda wa Polisi Ernest Mangu akisalimiana na Jenerali Davis Mwamunyange.Hapa ni IGP Ernest Mangu, Jen. Mwamunyange akisalimiana na DC wa Kinondoni, Paul Makonda..Baadhi ya waalikwa walioshuhudia tukio hilo Ukumbi wa Diamond Jubilee, ikiwemo viongozi wa dini pamoja na wengine… Mwenye suti ya blue ni mfanyabiashara, Dr.Reginald Mengi.Dr.Reginald Mengi na Jenerali Davis Mwamunyange.Mzee John Malecela, Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba akimwangalia jeraha la mkononi Nape Nnauye.Dk. Magufuli akikabidhiwa Cheti na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva.. yuko pia Mama Samia Suluhu na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima.Picha ya kumbukumbu:Rais Kikwete, Mama Salma, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Dk. Magufuli, Mama Samia, Jaji Damian Lubuva, pamoja na Mama Janeth Magufuli.Viongozi mbalimbali wakiwa pamoja na waangalizi wa Kimataifa wa Uchaguzi.Rais JK pamoja na Dk. Magufuli na Mama Samia Suluhu.Marais na wake zao, Rais Kikwete, Dk. Magufuli, Mama Salma Kikwete na Mama Janeth Magufuli.Rais Kikwete, Spika Anne Makinda, Dk. Magufuli na Rais Mstaafu wa Nigeria, Goodluck Jonathan...Baadhi ya waandishi wa Habari pamoja na wanachama wa CCM mbele ya Ofisi Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba.Rais JK, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Spika Anne Makinda, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM, Dr. Mohamed Seif Khatibu.Dr. Magufuli mbele ya Camera za waandishi wa habari pamoja na wanachama wa CCM kwenye Ofisi za CCM mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam.Dk. Magufuli akionesha cheti chake alichopewa na Tume ya NEC.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTER FBYOUTUBE