Leo February 22, 2018 habari kutoka India ni kwamba Madaktari wamefanikiwa kumfanyia upasuaji wa ubongo kijana mmoja wa miaka 31 na kutoa uvimbe ambao umepimwa na kukutwa kuwa na kilo 1.8.
Inaelezwa kuwa upasuaji huo uliofanyika February 14, 2018 ulidumu kwa saa saba na inasemekana kuwa huo ndio uvimbe mkubwa zaidi ambao umewahi kutolewa kwenye ubongo wa binadamu duniani kote.
Inadaiwa upasuaji huo haukutangazwa mapema kutokana na kwamba Madaktari walihofia kuwa huenda haukuwa wa mafanikio. Mwanaume huyu ajulikanaye kama Santlal Pal, ameeleza kuwa ameishi na uvimbe huo kwa miaka mitatu.
Daktari Mkuu wa Upasuaji wa Mfumo wa Neva Dkt Trimurti Nadkarni ameliambia shirika la utangazaji la BBC kuwa kwa sasa kilichobaki ni kupona tu lakini maisha yake hayapo hatarini tena.
JPM kwenye Mkutano wa 19 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
IBADA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU AKWILINA