April 7 2016 ni siku ambayo jina la mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu liligonga headlines kwa kasi kutokana na taarifa za kifo chake kuenea mitandaoni, awali kulikuwa na uvumi kuwa Mh Lissu amepoteza maisha taarifa ambazo hazikuwa za kweli.
millardayo.com ilitafuta ukweli wa stori yenyewe kuhusiana na taarifa hizo za msiba, ukweli ni kuwa Tundu Lissu yupo hai sema kuna mtu ambaye amefariki jina lake linaishia na Lissu ila Tundu Lissu yupo hai. Kaimu katibu mkuu wa CHADEMA Salum Mwalimu ameeleza ukweli wa taarifa hizo.
“Ni kweli tumepokea msiba wa aliyekuwa mbunge wetu wa viti maalum Singida Christina Lissu ambaye amefariki leo katika hospitali ya Aga Khan, Lissu atakumbukwa kwa umahiri wake wakati akiwa mbunge wa viti maalum katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015” >>> Salum Mwalimu
Kama utakuwa unakumbuka vizuri marehemu Christina Lissu aliwahi kuwa mbunge wa viti maalum kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kuanzia mwaka 2010 hadi 2015. Christina Lissu ni dada wa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE