Ni zaidi ya wiki moja na nusu kumekuwa na habari zikichukua uzito kwenye vyombo vya habari kuhusu mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Geita, Marehemu Alphonce Mawazo… kilichochukua muda mrefu zaidi ni ishu ya agizo la Kamanda wa Polisi Mwanza kuzuia CHADEMA kutofanya shughuli za kuaga kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mlipuko wa kipindupindu.
Mahakama Kuu kanda ya Mwanza iliruhusu CHADEMA kufanya taratibu za kuaga na mazishi, leo viongozi wa CHADEMA wamekutana Mwanza na kutoa ratiba nzima walivyojipanga na shughuli zote mpaka mazishi >>> “Tunaishukuru na kuipongeza Mahakama kwa sababu imani na tumaini letu ilikuwa ni Mahakama, tuliamini kwamba Mahakamani tafsiri ya Sheria itapatikana.”- Salum Mwalimu.
Kwenye sentensi nyingine za Salum Mwalimu >> “Tunalishukuru pia Jeshi la Polisi, jana baada ya kutoka Mahakamani tulikutana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza… Kikao kilitumia kama dakika 20, Kamanda wa Polisi akasema hana kinyongo na yuko tayari kutoa ulinzi wakati wote… Tunaamini kwa ushirikiano alioahidi kila kitu kitaenda kwa amani.”
Kuhusu taratibu za mazishi, mipango yao iko hivi >>> “Ilikuwa taratibu za kuaga na mazishi zianze leo lakini tumepata kibali leo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilemela, kibali kimeruhusu tuutumie uwanja wa Furahisha kwa siku ya kesho Jumamosi kuanzia saa tatu asubuhi.”
Kuhusu Ratiba ya kuaga na mazishi, Salum Mwalimu anaendelea kuelezea hapa >>> “Kesho saa mbili na nusu asubuhi tutatoa mwili wa marehemu Mawazo Hospitali ya Bugando Mwanza, tutaelekea nyumbani kwa baba mdogo kwa taratibu za kifamilia… baada ya kuaga, saa sita mchana tutaelekea viwanja vya Furahisha kwa ajili ya ibada, salamu za rambirambi… baada ya hapo tutaanza safari ya Geita.”
“Kesho kutwa tutaanza na ibada, salamu za rambirambi pamoja na taratibu nyingine mpaka mazishi Kijijini kwao Geita.”- Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar.
Sauti yote ya Salum Mwalimu hii hapa ikiwa na taarifa yote kutoka Mwanza.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.