Tukiwa bado akili na macho ya watanzania wengi yapo katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 Urusi, ambapo Taifa Stars itacheza mechi ya kwanza na Algeria November 14 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, shirikisho la soka ukanda wa Afrika Mashariki na kati (CECAFA) limetangaza Makundi matatu ya timu zitakazocheza michuano ya Challenge inayotarajia kuanza November 21 na kumalizika December 6.
KUNDI A
- Ethiopia
- Tanzania
- Zambia
- Somalia
KUNDI B
- Burundi
- Djibouti
- Kenya
- Uganda
KUNDI C
- Rwanda
- Sudan
- Sudan Kusini
- Zanzibar
Hata hivyo ratiba ya michuano hiyo bado haijatoka zaidi ya CECAFA kutangaza tarehe ya kuanza kwa michuano hiyo itakayofanyika Ethiopia. Timu ya taifa ya Kenya ndio Mabingwa watetezi wa Kombe hilo ambalo walitwaa mara ya mwisho mwaka 2013 Nairobi kwa kuifunga Sudan.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.