Michuano ya Kombe la Challenge 2015 imeendelea tena leo November 28 Ethiopia kwa timu kumaliza michezo yake ya hatua ya makundi, timu ya taifa ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars ilishuka dimbani kupambana na mwenyeji wa mashindano hayo timu ya taifa ya Ethiopia.
Kilimanjaro Stars walishuka dimbani kupambana na Ethiopia wakiwa na uhakika wa kutinga katika hatua ya robo fainali, kwani tayari walikuwa wamevuna point sita katika michezo yake miwili ya awali, ila Ethiopia ndio walikuwa na presha ya kuhitaji point angalau moja ili waweze kufuzu. Mchezo ulizidi kuwa mgumu na presha kwa Ethiopia baada ya Kilimanjaro Stars kupana goli la kwanza.
Stars walipata goli la kwanza dakika ya 52 baada ya Mohamed Hussein kupiga krosi safi iliyotiwa wavuni kwa kichwa na winga mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva na kufanya hali izidi kuwa ngumu kwa Ethiopia hadi pale walipoongeza mashambulizi dakika za nyongeza, Salim Mbonde akajifunga goli kwa bahati mbaya na kuisaidia Ethiopia. kwa matokeo hayo Kilimanjaro Stars itacheza tena na Ethiopia katika mchezo wa robo fainali.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.