Kuelekea uchaguzi mdogo February 17, 2018, Jeshi la Polisi la Mkoa wa Kinondoni limezungumza na waandishi wa habari na kutoa wito kwamba watu wafanye kampeni za kistaarabu zinazofuata misingi ya kisheria, kanuni na taratibu zilizoidhinishwa na Tume ya Uchaguzi.
Kamanda wa Polisi Kinondoni Murilo Jumanne Murilo ameeleza kuwa Jeshi la Polisi liko tayari kwa ulinzi, na litahakikisha kuwa sheria zinafuatwa, na pindi ukitokea ukiukwaji wa sheria, sheria yenyewe itawaelekeza nini cha kufanya.
“Suala la kampeni sio geni, linafanyika kwa misingi ya kisheria, zipo sheria zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi, jukumu letu ni kuhakikisha kuwa usalama unaimarika, wafanye kampeni za kistaarabu na za kufuata sheria.” – Kamanda Murilo
BREAKING: Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Butiama