Leo June 29 2016 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetengua matokeo ya ushindi yaliyompa Ubunge, Onesmo Nangole ‘CHADEMA’ jimbo la Longido kutokana na udanganyifu.
Akisikiliza kesi hiyo Jaji Sivangilwa Mwangesi amesema fomu zilizotumika kuandika matokeo ni fomu 21b za udiwani badala ya kutumia fomu 21c za ubunge hivyo uchaguzi utarudiwa.
Kesi hiyo ilifunguliwa mnamo June 29 2016 mahakama kuu Arusha na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ jimbo la Longido Dk. Steven Kiruswa.
Baada ya ushindi wa kesi hiyo dhidi ya Onesmo Nangole ‘CHADEMA’ Dk. Kiruswa ‘CCM’ amesema…..>>>’tunangojea wenzetu kama wana sababu ya kukata rufaa, wakate baada ya hapo tutaenda uwanjani kuanza upya….tulikuwa na madai mengi ya msingi lakini moja ni kuwepo kwa kasoro katika utaratibu waliotumia kuhesabu, kujumlisha na kutangaza matokeo ya uchaguzi‘
ULIPITWA NA HII YA TUNDU LISSU KUFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU TUHUMA ZA UCHOCHEZI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE