CHADEMA wamemteua Sharifa Suleiman kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chama hicho (BAWACHA) ambapo kabla ya uteuzi huo, Sharifa alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo.
Akizungumza katika kikao cha kuchagua Viongozi wa Chama hicho kujaza nafasi zilizoachwa wazi, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema kutokana na Sharifa kutosaliti wala kuhasi chama, Kamati Tendaji ya CHADEMA wamempitisha kukaimu nafasi hiyo mpaka watakapoitisha uchaguzi.
“Kuna jambo jingine ambalo ofisi ya katibu mkuu na Bawacha tulifikiria lifanywe na Bawacha, mchakato wake wa kukaimisha kwa muda zile nafasi nyingine zilizo wazi ambazo hamna mamlaka ya kikatiba ya kumchagua kuziba moja kwa moja.” Mnyika
“Kwa uamuzi huo hatutokaimisha nafasi hizo kwenye kikao hiki badala yake Chadema ina utajiri mkubwa wa taratibu za uendeshaji wa chama. kwa uamuzi wa kamati kuu tunapenda kutumia kifungu cha 12(0) cha itifaki ya chama ambayo kifungu cha 12.12 (2) kinasema yafuatayo na naomba ninukuu” Mnyika
“Makamu wenyeviti watakuwa wasaidizi wakuu wa wenyeviti na kazi zao na kukaimu wakati ambapo wenyeviti hawapo, kwakuwa hakuna mwenyekiti, makamu mwenyekiti alibaki ambaye hakushiriki usaliti, uhasi na ubinafsi sasa yeye atakaimu uenyekiti mpaka pale tutakapoitisha mchakato wa uchaguzi wa kuziba nafasi,” Mnyika.