NI Julai 27, 2023 ambapo Chama cha waagizaji na wasambazaji wa Mafuta Tanzania TAOMAC wamefunguka haya kuhusu sakata la wa Mafuta nchini.
‘Tumebaini kuwepo kwa taarifa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii ikidai kuwa waagizaji na wasambazaji wa mafuta wamekaa kwenye kikao na EWURA na kuishia kwenye mtafaruku na kutokukubaliana’-
‘Kwa niaba ya Wanachama wetu wa Chama cha Waagizaji na Wasambazaji wa Mafuta Tanzania (TAOMAC) ambao wanajumuisha zaidi ya 97% ya soko la mafuta yanayoingizwa nchini, tunapenda kukanusha taarifa hizi kwa kuwa sio za kweli.Hatujaakaa kikao na EWURA kwa zaidi ya wiki mbili.Pia hatujawahi kukaa kikao na EWURA na kuishia kwa mtafaruku.Aidha, sekta ya uagizaji na usambazaji wa Mafuta inapitia changamoto ya Ukosefu wa Dola, lakini tumeshakaa vikao na mamlaka zinazohusika na tumeahisiwa kuwa tatizo hili linafanyiwa ufumbuzi.Wanachama wetu wanaendelea kuagiza mafuta na wataendelea kufanya hivyo ili hakikisha nchi haikosi Mafuta’