Ongezeko la utoroshwaji wa mazao ya Nigeria kwenda nchi jirani limeongeza changamoto ya mfumuko wa bei ya chakula nchini humo huku serikali ikijaribu kupunguza hali hiyo kwa kuziba mianya ya mpaka.
Malori ya nafaka na vitu vingine vinaripotiwa kusafirishwa kutoka Nigeria hadi nchi jirani kupitia njia za siri katika majimbo hata wakati wananchi wakikabiliana na hali mbaya ya kulimbikiza na kupanda kwa mfumuko wa bei ya vyakula.
Uzito wa hali hiyo unaakisiwa na Makamu wa Rais Kashim Shettima kukiri waziwazi kudorora kwa chakula katika mkutano wa usimamizi wa mali mjini Abuja Februari 20.
“Siku tatu tu zilizopita, lori 45 za mahindi zilinaswa zikisafirishwa hadi nchi jirani,” Shettima aliuambia mkutano. “Wakati ambapo vyakula vilizuiliwa, bei ya mahindi ilishuka kwa N10,000…Kuna nguvu zinazolenga kuhujumu taifa letu.”
Kabla ya hotuba ya Makamu wa Rais kwenye hafla hiyo, forodha ya Nigeria iliripoti kukamata mizigo ya vyakula ambayo mashirika ya magendo yalikuwa yakijaribu kupitia njia kadhaa, likiwemo Jimbo la Jigawa kaskazini-magharibi mwa nchi.