Mwanamke mmoja nchini Marekani anaefahamika kwa jina la Jeniffer Haller mwenye umri wa miaka 43 amekubali kufanyiwa majaribio ya dawa itakayotumika kama chanjo ya virusi vya corona, Jennifer ni Mama wa Watoto wawili lakini anasema licha ya kufahamu kuwa jaribio hilo ni hatari ameamua kujitoa kulifanya ili kuiokoa Dunia.
“Ninaifurahia hii fursa ya kufanya kitu kikubwa kitakachoisadia jamii kwa vizazi vya leo na kesho pia kama chanjo itafanikiwa”– JENIFFER
Watu kibao akiwemo Rais wa Marekani Donald Trump wameonesha hisia zao kwa namna walivyoguswa na alichokifanya jeniffer.