Mwanzilishi wa Taasisi ya Charming charity organization Ndg. John Mkonyi ameitaka jamii kuendelea kuwakumbuka Watoto wenye uhitaji mkubwa, hasa wale wanaoisha kwenye mazingira magumu lakini pia hata wale Watoto Yatima.
Mwanzilishi huyo ameyazungumza hayo hii leo February 25, 2023 wakati wakitoa msaada wa mahitaji tofauti tofauti kwa Kituo cha Watoto Yatima Umra kilichopo Magomeni, Mikumi Jijini Dar es Salaam huku akiwa ameongozana na baadhi ya Wadau wa Taasisi hiyo ya Charming Charity Organization.
“Tuungane pamoja kuendeleza harakati za kuwasaidia wale wote wenye Uhitaji, hasa hawa Watoto yatima kwani walitamani kuwa na Wazazi wao lakini leo hii haipo hivyoo, sisi Kama Charming Charity Organization tumeliona hilo na ndio maana tumeamua kufanya” Amesema Mwanzilishi Ndg. John Mkonyi.
Hata hivyo kwa Upande wa Kituo hicho wameshukuru sana ujio wa Taasisi hiyo hapo kwani kwao imekuwa ni faraja kubwa kwa upande wao nao imezidi kuwaongezea Furaha watoto hao pamoja na Walezi wa kituo hiko.
” Tunashukuru Mungu, lakini pia tunaishukuru Taasisi ya Charming Charity Organization kwa kuja kututembelea hapa kwetu na kutuletea baadhi ya mahitaji muhimu kwa Watoto wetu hawa Sisi kama Umra tumefurahi na tunazidi kuwakaribisha wengine nao waje kututembelea” Ameyasema hayo Mama Mlezi wa Kituo cha Umra Rahma Kishumba.