Jijini Dar es salaam kumekuwa na zoezi la kuwaondoa ombaommba ambalo limekuwa likitekelezwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ikiwa ni utekelezaji wa agizo la kuwaondoa lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Baada ya zoezi hilo leo July 29 2016 Chama cha Walemavu mkoa wa Dar es salaam kimeiomba Serikali kusitisha zoezi hilo kwa ombaomba ambao ni wenye ulemavu ndani ya mkoa wa dar es salaam badala yake serikali itatue changamoto zinazowakabili kwa kuwawezesha mitaji ya biashara na kwa wale wenye elimu wapatiwe kazi kuendana na sifa zao.
Akizungumza na Ayo TV jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa chama cha walemavu mkoa wa Dar es salaam, Hamad Komboza amesema……
>>>si kwamba tunawaunga mkono waendelee kuomba, hapana sisi tunaiomba serikali katika kuwakamata ombaomba kuwe na tija kwa maana sisi wenye ulemavu tunazo changamoto nyingi zinazotusababishia sisi kuomba na kama zikiondolewa hakuna mtu mwenye ulemavu atakayeonekana barabarani akiomba‘
ULIKOSA MATATU YA RAC MAKONDA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI