Mkuu wa wilaya ya Bukombe Mh.Said Nkumba Leo akiwa wilayani Chato Mkoani Geita amefungua Rasmi Mashindano ya Michezo mbalimbali ya Samia Cup 2023 yaliyoandaliwa na Wadau mbalimbali wa Maendeleo wilayani humo kwa kushirikiana na Mkuu wa wilaya ya Chato.
Akizungumza katika Ufunguzi huo uliofanyika katika Tarafa ya Mganza wilayani humo akimwakilisha Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma amesema Lengo la Michuano hiyo ni kuibua na kukuza vipaji vinavyopatikana katika wilaya ya Chato huku akiitaka Jamii kutobedha Baadhi ya Michezo .
“Mmeingia kwenye haya mashindano Matumaini yangu Mtashindana Timu zitakuwa nyingi lengo kubwa ni kukuza Vipaji netball ni Moja ya Mchezo ambao ukicheza vizuri unaweza ukachukuliwa ukaenda kwenye Timu zingine za Maeneo mbalimbali kutimiza ndoto ambayo unayo ,” Mwakilishi Naibu wa Utamaduni Sanaa na Michezo.
Nkumba amesema katika Mashindano hayo pia yanasaidia kuuunga Jitihada zinazo fanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuinua Sekta ya Michezo hapa Nchini ikiwemo Mpira wa Miguu ,Mpira wa Netball na Masumbwi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Chato,Deusdedith Katwale amesema Mashindano hayo yameandaliwa na Wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Ofisi yake katika kusaidia vijana ambao hawana ajira kuonyesha Vipaji vyao na kuepukana na vitendo vya Uharifu ndani ya wilaya hiyo.
Katika hatua nyingine Katwale amesema pia tengo la Mashindano hayo ni katika kuhamasisha Shughuli za Maendeleo kwa wananchi wajikite zaidi katika kilimo huku akimpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuunga shughuli za Kimichezo ambazo zimekuwa zikiendelea katika maeneo mbalimbali ya Nchi.